Tokyo: Mtu mkongwe kabisa afariki
13 Novemba 2003Matangazo
Mtu mzee kabisa dunia, Mitoyo Kawate, alifariki nchini Japan hii leo akiwa na umri wa miaka 114, wiki mbili baada ya kuteuliwa. Kawate alifariki kwa homa ya mapafu hospitalini, katika mji wa kusini magharibi wa Hiroshima, afisa wa wizara ya afya alisema. Haikujulikana papo hapo ni nani sasa mtu mzee kabisa duniani. Afisa wa wizara alisema kwamba mwanamke mkongwe kabisa nchini Japan sasa ana umri wa miaka 113 Bibi Ura Koyama, anayeishi katika mji wa kusini magharibi wa Fukuoka.