1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Mjapani atekwanyara nchini Iraq

10 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFF4

Waziri wa kigeni wa Japani,Nobutaka Machimura amethibitisha kuwa mfanyakazi mmoja wa Kijapani katika kampuni ya kigeni inayohudumia usalama ametekwa nyara nchini Iraq.Hapo kabla kikundi kimoja cha wanamgambo wa kiislamu kilisema kuwa kimemzuia raia mmoja wa Kijapani anaefanya kazi kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Iraq.Kwa wakati huo huo kiongozi wa kiislamu kutoka Australia ameondoka Sydney kwenda Iraq kujaribu kupata uhuru wa Muaustralia mmoja aliezuiliwa mateka,zaidi ya wiki moja.Wateka nyara wa Douglas Wood mwenye umri wa miaka 63,wametishia kuwa watamuuwa ikiwa vikosi vya Australia na vya washirika wengine havitoondoka Iraq.