1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Marekani na China zafanya juhudi mpya za kuyafufua mazungumzo na Korea Kazkazini

10 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8n

Marekani na China zimepiga hatua mpya za kidiplomasia leo kuyaanzisha tena mazungumzo na Korea Kazkazini, ambayo imeonya iko tayari kwa vita baada ya kuyafanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu.

Huku baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kuamua baadaye leo lini litakapolipigia kura azimio linalonuia kuiadhibu Korea Kazkazini, wajumbe wa Marekani na China walifanya mazungumzo nchini Japan na Korea Kazkazini.

Kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan, Taro Aso, mjini Tokyo, naibu waziri anayeshughulikia maswala ya Asia Mashariki wa Marekani, Christopher Hill, amesema Korea Kazkazini inalazimika kuchagua kati ya kuendelea kutengwa na jamii ya kimataifa na kujiunga na jumuiya hiyo.

Hill ameionya Korea Kazkazini akisema, ´Tunataka ifahamike wazi kwamba sote tunapinga kwa kauli moja hatua ya uchokozi ya Korea Kazkazini kufanyia majaribio makombora yake.

meongeza kusema kuwa makombora haya hayalengi tu kuitisha Marekani bali pia washirika wake na kuvuruga amani kazkazini mashariki mwa Asia.

Japan leo imefutilia mbali mpango wake wa kushurutisha kura ipigwe juu ya vikwazo dhidi ya Korea Kazkazini kufuatia juhudi mpya za kidplomasia. China na Urusi, ambazo zina kura ya turufu, zinalipinga azimio hilo.