TOKYO: Majadiliano kuendeleza uchumi wa Wapalestina
14 Machi 2007Matangazo
Wajumbe wa Israel na wa Wapalestina wamekutana katika mji mkuu wa Japan,Tokyo kujadiliana njia za kuendeleza uchumi wa Wapalestina.Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni kuanzishwa mradi wa kilimo na viwanda katika Ukingo wa Magharibi. Majadiliano hayo yamehudhuriwa pia na Makamu Waziri Mkuu wa Israel,Shimon Peres na mpatanishi mkuu wa Wapalestina Saeb Erekat.Majadiliano ya Tokyo yanatazamwa kama ni sehemu ya juhudi za kuanzisha upya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.