1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Mahkama yatupilia mbali kesi ya fidia ya Wachina

19 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLc

Mahkama ya Japani imezidi kuongeza mvutano kati ya nchi hiyo na China kwa kutupilia mbali kesi ya fidia iliowasilishwa na wahanga 10 wa China walionusurika na unyama wa Japani ikiwa ni pamoja na mauaji ya Nanjing ya mwaka 1937 wakati wanajeshi wa Japani walipokuwa wakikalia kwa mabavu sehemu kubwa ya China.

Mahkama Kuu ya Tokyo imegoma kusikiliza rufaa hiyo ya wanawake 10 wa China.Hatua hiyo inafuatia maandamano dhidi ya Japani katika miji ya China kupinga kile kinachonekana kuwa ni kushindwa kwa Japani kujutia matendo yake ya zamani wakati wa vita pamoja na vitabu vya kusomea nchini Japani vyenye utata.

Japani inataka China iombe radhi kutokana na uharibu uliofanywa na waandamanaji kwa balozi zake ndogo nchini China.