1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Kundi la mwanzo la wanajeshi 30 wa Japan linaondoka leo kuelekea ...

16 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFii
Iraq kujiunga na wanajeshi wa nchi shirika wanaoongozwa na Marekani.Waziri mkuu Junichiro Koizumi amehakikisha wanajeshi wa nchi yake hawatoshiriki vitani,wala katika opereshini nyenginezo za kijeshi.Bunge la Japan lilibidi kuifanyia marekebisho katiba kuweza kuruhusu wanajeshi wa Japan watumwe nchini Iraq.Uamuzi kuhusu kutumwa wanajeshi 600 wa Japan nchini Iraq unatarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.Utategemea ripoti ya uongozi wa kijeshi kama mahala watakakowekwa wanajeshi hao ni salama au la.Japan ikizingatia mafungamano yake na Marekani imependekeza kutuma hadi wanajeshi 1000 nchini Iraq.Kundi hilo la mwanzo litazamiwa kuwasili Kuweit kesho kabla ya kuelekea Samaua kusini mashariki ya Iraq mwioshoni mwa mwezi huu.Wanajeshi wa Japan wamepangiwa kushughulikia huduma za jamii na kusaidia kulijenga upya eneo hilo.