1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Kundi la kwanza la wanajeshi wa Japan limeondoka Tokyo ...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFp7

kuelekea Iraq.Wanaanga 40 wa mwanzo wanaelekea kwanza Kuweit.Wanatazamiwa kusafirisha misaada ya madawa na chakula toka Kuweit hadi katika viwanja vya ndege vya Baghdad,Basra,Balad au Mossul.Wanajeshi hao wa mwanzo wa Japan wamepangiwa pia kutathimini hali ya mambo kabla ya wanajeshi zaidi kutumwa katika eneo hilo.Kundi la pili na kubwa la wanaanga wa Japan linatazamiwa kuwasili mwezi ujao.Hii ni mara ya kwanza tangu vita vikuu vya pili vya dunia kumalizika kwa Japan kutuma wanajeshi katika nchi inayogubikwa na mapigano.