1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Koizumi asomba ushindi mkubwa

11 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcD

Chama tawala cha muda mrefu nchini Japani cha Waziri Mkuu Junichiro Koizumi kimezowa ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa baraza la chini la bunge uliofanyika nchini humo leo hii.

Matokeo ya awali kwa mujibu wa televisheni yanaonyesha ushindi mkubwa kwa chama hicho ambao utampa mamlaka makubwa Koizumi kwa ajili ya mageuzi yanayopendelea uchumi wa nguvu za soko.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yaliotolewa na Shirika la Utangazaji la taifa NHK yameonyesha kwamba chama cha Liberal Demokratik LDP ambacho kimekuwa kikiongoza nchi hiyo kwa serikali ya mseto kitajishindia kati ya viti 285 hadi 325 katika baraza hilo la bunge lenye viti 480.NHK pia imetabiri kwamba chama cha LDP na washirika wake Chama cha New Komeito vitashinda jumla ya viti kati ya 313 na 361 kwa pamoja na kuviwezesha kulidhibiti baraza la chini la bunge kwa mara ya kwanza kabisa katika kipindi cha miaka 15.

Matokeo hayo ya awali ya uchaguzi yanaonyesha chama cha msimamo wa wastani cha Demokrasia ya Japani ambacho ni chama kikuu cha upinzani kimejipatia kati ya viti 84 hadi 127.

Koizumi ameitisha uchaguzi huo wa ghafla baada ya mpango wake wa mageuzi wa kuligawa na kulibinafsisha shirika la Posta la Japani kukataliwa katika baraza la chini la bunge