1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Koizumi anaongoza kura ya maoni.

10 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcd

Katika mkesha wa uchaguzi nchini Japan , maoni yanaonyesha kuwa chama cha waziri mkuu Junichiro Koizumi cha Liberal Democratic , LDP, kinaongoza.

Bwana Koizumi aliitisha uchaguzi huo ili kuweza kusukuma mbele mipango yake ya ubinafsishaji wa shirika la posta nchini humo.

Waziri mkuu amesema kuwa hatua hiyo itatia msukumo mpya katika uchumi wa Japan na kusafisha utamaduni wa kisiasa nchini humo wa upendeleo.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Party of japan DJP, wakati huo huo , kinaahidi mageuzi makubwa na kudai kuwa Koizumi ameshikilia tu suala la ubinafsishaji wa shirika la posta, ambalo kwa hakika benki yake ndio kubwa kabisa duniani.

Posta Japan ina mali zinazofikia kiasi cha dola trilioni tatu, na matawi 25,000 ambayo ni pamoja na benki na bima.