TOKYO: Kimbunga kikali kinaelekea mji mkuu wa Japan
15 Julai 2007Matangazo
Kimbunga kikali kabisa kupata kutokea tangu miongo mitatu sasa kinaelekea mji mkuu wa Japan, Tokyo.Siku ya Jumamosi,kimbunga Man-yi kilivuma kwenye visiwa vikuu vya Kyushu na Shikoku kusini na kusini-magharibi ya nchi.Watu watatu wamepoteza maisha yao na mmoja hajulikani alipo. Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha,yamesomba idadi kadhaa ya nyumba na maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao. Kimbunga Man-yi kinaelekea Tokyo,kwa mwendo wa kilomita 162 kwa saa.