1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Kagame ataishia kuvamia Congo

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCup

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema leo hii yuko tayari kutuma tena vikosi vyake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iwapo nchi hiyo itashindwa kuwadhibiti wanamgambo.

Lakini amesema kwamba kwa hivi sasa anasubiri matokeo ya uchaguzi wa kihistoria katika nchi hiyo jirani ilioathirika na vita.

Akizungumza akiwa ziarani nchini Japani Kagame amesema iwapo watashambuliwa na wanamgambo au na mtu yoyote yule watakuwa na haki na uwezo wa kukabiliana na tatizo hilo.

Kagame alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa mjini Tokyo ambapo pia amesema watafanya kile nchi yoyote ile itafanya ikiwa inashambuliwa na huo ndio ukweli wa mambo ulivyo.