TOKYO : Japani yapata mrithi wa ufalme
6 Septemba 2006Binti Mfalme wa Japani Kiko amejifunguwa mtoto wa kiume leo hii akiwa ni mrithi wa kwanza wa kiume kuzaliwa katika ukoo wa kifalme katika kipindi cha zaidi ya miongo minne na kuwa jibu la dua za wahafidhina ambao wamekuwa na shauku ya kuwaweka kando wanawake katika kiti cha enzi cha kale.
Kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume kutasitisha kwa hivi sasa mpango wa kuwawezesha wanawake kurithi kiti hicho cha ufalme wazo ambalo limekuwa likipingwa na wahafidhina wanaotaka kudumisha mtindo ambao wanasema umeanzia zamani sana zaidi ya miaka 2,000 iliopita.
Jambo hilo linaweza kuwavunja moyo Wajapani wengi ambao walikuwa wakipendelea kupatiwa haki sawa kwa wanawake.
Magazeti leo yametowa matoleo ya ziada kutangaza kuwasili kwa mjukuu wa kwanza wa kiume wa mfalme.