TOKYO: Japan yatangaza tahadhari ya kimbunga cha Tsunami.
13 Januari 2007Matangazo
Japan imetoa tahadhari ya kimbunga cha Tsunami pwani ya eneo la kaskazini la Hokkaido na pia kwenye kisiwa cha Honshu baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika bahari ya Pasifik.
Maafisa wa serikali wamesema mawimbi makubwa yamegonga eneo hilo kutokana na tetemeko hilo lililokuwa na uzito wa nane nukta tatu katika vipimo vya Richter.
Hapakuwa na taarifa za kuwepo majeruhi.
Marekani pia imetoa tahadhari tofauti ya kimbunga cha Tsumani kwa Russia, Japan na kisiwa cha Markus katika bahari ya Pasifik.