TOKYO: Japan yataka utulivu.
11 Aprili 2005Matangazo
Japan imetoa mwito wa utulivu na kuanzishwa mazungumzo ya pamoja na China kufuatia maandamano makubwa dhidi yake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini China.
Tokyo imewataka pia viongozi wa Beijing waombe radhi na kuhakikisha usalama wa raia na wanadiplomasia wake baada ya visa hivyo vya ghasia ambako waandamanaji walihujumu maduka na taasisi za Japan nchini China.
Hasira za Wachina dhidi ya Japan zimepata nguvu baada ya utawala wa Japan kuchapisha kitabu cha historia kinachokana madhila yaliyotekelezwa na Japan katika vita vikuu vya pili vya dunia.
Viongozi wa Beijing wanapinga pia juhudi za Japan za kugombea kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.