1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Japan yarefusha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

10 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAz

Japan imeamua hii leo kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini vilivyowekwa mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kufanya jaribio la kombora la nyuklia, huku kukiwa na wasiwasi kwamba serikali ya Pyongyang huenda isikifunge kinu chake cha nyuklia kufikia katikati ya mwezi huu.

Vikwazo hivyo, vinavyojumulisha marufuku ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Korea Kaskazini na ambavyo vinazipiga marufuku meli zote za Korea Kaskazini kuingia bandari za Japan, vitarefushwa kwa miezi sita.