1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Japan imetuma kundi la mwanzo la askari 20 kushughulikia...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFoy

misaada ya kiutu nchini Iraq.Kundi hilo litawekwa kwanza kusini mwa Iraq kunakotajikana ni salama.Wanajeshi elfu moja zaidi wa Japan watafuata.Lengo la shughuli hizo kubwa kabisa kuwahi kusimamiwa na wanajeshi wa Japan tangu vita vikuu vya pili vya dunia vilipomalizika,ni kusaidia katika huduma za afya,ujenzi wa shule,mitambo ya kusambaza maji na huduma nyenginezo za jamii.Sheria maalum ilibidi kuidhinishwa na bunge la Japan july iliyopita ili kuviruhusu vikosi vya nchi hiyo kuwekwa nchini Iraq.Sheria hiyo inasisitiza vikosi vya Japan viwekwe katika eneo salama na visihusishwe na mapigano.