1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Dr.Condoleezza Rice azitembelea nchi za Asia

19 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVX

Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ameitaka Korea ya Kaskazini moja kwa moja irejee kwenye majadiliano yanayohusika na miradi yake ya kinuklia.Akizungumza katika Chuo Kikuu mjini Tokyo-Ujapani,Dr.Rice kwa mara nyingine tena amesema Marekani "haina azma ya kuishambulia au kuivamia Korea ya Kaskazini." Akaongezea kuwa Washington ipo tayari kuihakikishia Korea ya Kaskazini usalama wake kwa kuzihusisha pande mbali mbali,ikiwa itasitisha mpango wake wa kinuklia.Pyongyang imekataa kufanya majadiliano zaidi na Washington,ikimtaka Rice kwanza aombe msamaha kuhusika na matamshi kuwa Korea ya Kaskazini ni "ngóme ya udhalimu."Rice akiendelea na ziara yake barani Asia,ametoa muito vile vile kwa Uchina kufanya mageuzi zaidi ya kidemokrasia.Uchumi wa Uchina unaostawi lazima uende sambamba na uhuru zaidi wa kisiasa alieleza Bibi Rice.