1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Bunge laidhinisha mageuzi

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CES4

Nchini Japani baraza la juu la bunge limeidhinisha muswada ambao utapelekea kubinafsishwa kwa huduma za posta za taifa.

Mpango huo ni sehemu ya mageuzi makubwa ya huduma za taifa ya Waziri Mkuu Junichiro Koizumi.Hapo mwezi wa Augusti baraza hilo la juu la bunge liliukataa muswada huo na kusababisha kuitishwwa kwa uchaguzi mkuu na mapema ambao chama cha LDP cha Koizumi kilishinda.

Chini ya mageuzi hayo Shirika la Posta la Japani litagawiwa sehemu mbili tafauti ambapo hatimae kutapelekea kuanzishwa kwa benki kubwa kabisa ya akiba duniani.