1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Askari wa Japani waenda Iraq

25 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpW


Kundi la kwanza la askari 40 wa Japani wanaondoka ijumaa kuelekea Iraq kujiunga na harakati za ujenzi mpya wa nchi hiyo. Taarifa za serikali mjini Tokyo zimearifu kuwa kikundi hicho kimetumwa kuandaa mipango ya mapokezi ya maafisa wa Japani watakaohusika na shughuli za utoaji wa misaada ya dharura nchini humo. Japan inapanga kutuma askari wake wapatao 1000 kwenda Iraq kusaidia kazi za ujenzi mpya wa nchi hiyo na ambao watakuwa wanajeshi wa kwanza wa Japani kutumwa katika eneo lenye vita tangu kumalizika vya pili vya dunia. Kimsingi katiba ya Japani inapinga matumizi ya nguvu katika ufumbuzi wa mizozo ya kimataifa.