1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Abe achaguliwa kuwa kiongozi wa LDP

20 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAb

Shinzo Abe amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala nchini Japani cha LDP.

Hatua hiyo inatoa nafasi kwa Abe kuwa waziri mkuu mpya wa Japani hapo wiki ijayo.Alijizolea kura 464 wakati mpinzani wake wa karibu Waziri wa mambo ya nje Taro Aso alijipatia kura 136.

Abe ameahidi kuifanya Japani kuwa mtendaji shupavu katika jukwaa la kimataifa na anakusudia kuimarisha uhusiano madhubuti wa usalama na Marekani wakati akichukuwa msimamo mkali dhidi ya Korea Kaskazini.

Iwapo atachaguliwa wiki ijayo atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Japani kuzaliwa baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.