1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKIO: Korea ya Kaskazini kufunga mtambo wa nyuklia

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpA

Korea ya Kaskazini na Marekani zimekubaliana kufunga mtambo wa nyuklia wa Yongbyon katika kipindi cha majuma matatu yajayo.Hayo alitamka naibu waziri wa nje wa Marekani,Christopher Hill alipozungumza na waandishi wa habari mjini Tokio. Amesema,wakaguzi wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa watawasili Korea ya Kaskazini siku ya Jumanne. Wataalamu hao watafanya matayarisho ya kuufunga mtambo wa Yongbyon ambao ni kitovu cha mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Hiyo itakuwa ziara ya kwanza kufanywa na wakaguzi wa Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA-tangu miaka mitano iliyopita,baada ya kutimuliwa na kiongozi wa Korea ya Kaskazini,Kim Jong Il mwishoni mwa mwaka 2002.Mapema mwaka huu,katika majadiliano ya pande sita juu ya mzozo wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini,mojawapo ya vifungu vya makubaliano yaliyofikiwa,ni kuufunga mtambo wa Yongbyon.