1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tishio la kigaidi katika mataifa ya Kiarabu na Asia

4 Agosti 2013

Marekani imefanya mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu kufuatia wasiwasi wa kutokea vitendo vya kigaidi, ambavyo vimesababisha serikali ya taifa hilo kutoa tahadhari ya kusafiri na kuamuru kufungwa kwa balozi zake.

https://p.dw.com/p/19JRq
U.S. Ambassador to the United Nations Susan Rice speaks to the media at the U.N. headquarters in New York February 12, 2013. The U.N. Security Council met in an emergency session on Tuesday for discussions on possible new sanctions against North Korea in retaliation for its third nuclear weapons test, an act Secretary-General Ban Ki-moon condemned as deplorable. REUTERS/Eduardo Munoz (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Susan RicePicha: Reuters

Mkutano huo umefanyika baada ya polisi wa kimatafa Interpol kutoa tahadhari ya kiusalama ya kimataifa, baada ya mamia ya wafungwa wenye mfungamano na kundi la al-Qaeda kutoroka katika magereza kadhaa katika mataifa manane tofauti na tukio la watu waliojitoa mhanga kusababisha vifo vya watu tisa karibu na ubalozi wa India huko mashariki mwa mji wa Jalalabad, nchini Afghanistan.

Rais Obama kaarifiwa kuhusu mkutano

Mkutano huo uliongozwa na Mshaauri wa Taifa wa Masuala ya Usalama wa Marekani, Susan Rice, umehudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje John Kery, Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel pamoja na Waziri wa Usalama wa Nchi, Janet Napolitano.

U.S. President Barack Obama speaks about the economy during a visit to Knox College in Galesburg, Illinois July 24, 2013. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS BUSINESS)
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: REUTERS

Ikulu ya Marekani imesema vilevile mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa CIA, FBI na wawakilishi kutoka usalama wa taifa hilo. Rais Barack Obama hakuhudhuria lakini aliarifiwa kile kilichojadiliwa katika mkutano huo.

Mapema wiki hii, rais Barack Oboma alitoa maelekezo kwa idara ya usalama wa taifa hilo kuchukua hatua kila inayowezekana kuwalinda raia wa Marekani pale panapotokea kitisho cha usalama wao katika maeneo waliyopo au hata kutoka katika rasi ya Uarabuni.

Amri ya kufungwa ofisi za Kibalozi

Kutokana na kitisho cha kutokea mashambulizi ya kigaidi Marekani imeamuru leo hii (04.08.2013) kufunga balozi zake. Mataifa mengine kama Ujerumani, Uingereza na Ufaransa wamfuata uamuzi huo na wapo katika hatua za kufunga balozi zake nchini Yemen kwa takribani siku mbili. Canada vilevile imesema itafunga ubalozi wake uliypo katika mji mkuu, Dhaka nchini Bangladesh.

Ijumaa iliyopita Marekani ilitoa onyo la kusafiri, kwa kuzingatia mpango ambao haujaweza kufahamika wa kushambulia Marekani katika maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Polisi ya kimataifa-Intepol imetoa tahadhari hiyo kufuatia kitendo cha kuvunjwa kwa magereza katika mataifa mananae tofauti likiwemo Libya, Iraq, na Pakistan. Tahadhari hiyo inasema mamia ya magaidi na wahalifu wengine wametoroka kutoka kwa mwezi uliyopita pekee.

Ofisi ya Intepol iliyopo mji wa Lyon, Ufaransa imesema mwezi wa nane, ni mwezi ambao kumefanyika mashambulizi ya kigaidi ya India, Urusi na Indonesia. Wiki hii vile vile kunaadhimishwa miaka 15 ya mashambulizi ya kigaidi ya Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania, ambayo zaidi ya watu 200, walifariki dunia na maelfu kujeruhiwa.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri: Kitojo Sekione