Timu zilizoingia nusu fainali kombe la dunia zakamilika
8 Julai 2018Chakula maarufu nchini Uingereza cha samaki na Chips dhidi ya chakula maarufu cha Croatia cha Samaki Risotto. Kinywaji cha Ufaransa cha Vin et fromage dhidi ya bia ya Ubelgiji.
Wenyeji Urusi waliondoka uwanjani usiku wa Jumamosi wakidondokwa machozi , baada ya kutoka sare dhidi ya Croatia kwa mabao 2-2 na mchezo huo kuingia katika dakika za nyongeza na hatimaye kushindwa kwa mikwaju ya penalti.
Wajurumani ambao huwa makini sana waliondolewa mapema, pamoja na kikosi cha Samba cha Brazil pamoja na tiki taka ya Uhispania.
Argentina ya Lionel Messi na Cristiano wa Ureno hawakuweza kuvuka kiunzi cha timu 16 bora. Azzurri ya Italia haipata hata fursa ya kualikwa hata kufikia katika awamu hii ya fainali.
"Yeyote ambaye alipigiwa upatu kutoroka na taji hili, timu vigogo , ziko nyumbani," kocha wa Croatia Zlatko Dalic alisema kupitia mkalimani. Wale waliofanya kazi kwa bidii , ambao wanacheza kama timu, wako pamoja na ambao wamejiandaa vizuri , bado wako hapa Urusi, na hii ndio hali ya timu nne zilizobakia katika kinyang'anyiro hiki."
Kinyang'anyiro cha kwanza kitakuwa kati ya Les Bleus dhidi ya De Rode Duivels siku ya Jumanne usiku mjini St. Petersburg, pambano la majirani kutoka bara la Ulaya.
Pambano kati ya Simba watatu dhidi ya Vatreni litafuatia usiku wa siku ya Jumatano mjini Moscow. Je kandanda linarejea nyumbani ama taji litakwenda sehemu nyingine mpya ?
"tumo katika nusu fainali ya kombe la dunia. Iwapo tumo katika timu nne bora duniani bado ni kitu ambacho tunapaswa kuthibitisha," Meneja wa England Gareth Southgate alisema. "Itakuwa ishara kwa vilabu vyote kwamba, iwapo ni England ama kwingineko, kwamba wachezaji wa Uingereza wanaweza kucheza soka, kwamba tuna wachezaji ambao wana ustadi mkubwa.
Timu bora za dunia ?
Katika orodha ya timu bora za shirikisho la kandanda duniani FIFA , mapambano hay ya nusu fainali hayalingani.
Ubelgiji iko katika nafasi ya tatu duniani, Ufaransa ya saba, England ya 12 na Croatia ya 20.
Ufaransa iliikandika Ubelgiji mabao 5-0 mjini Nantes katika awamu ya makundi mwaka 1984 katika ubingwa wa Ulaya wakati Michel Platini alipopachika mabao 3, na kisha kushinda kwa mabao 4-2 katika mchezo wa nafasi ya tatu wa kombe la dunia mwaka 1986 nchini Mexico baada ya Ubelgiji kushindwa katika nusu fainali na Argentina kwa mabao 2-0, ambapo Diego Maradona alipachika mabao 2.
Kizazi kimoja hapo kabla, Emile Veinante alipachika bao katika dakika ya mwanzo ya mchezo ambapo Ufaransa ilishinda mabao 3-1 mjini Paris katika duru ya timu 16 bora katika fainali za kombe la dunia mwaka 1938.
Tangu kushinda taji lake pekee katika uwanja wa Wembley mwaka 1966, England ilifika awamu ya nusu fainali mara moja tu, na kushindwa na Ujerumani ya magharibi wakati huo kwa mikwaju ya penalti katika fainali zilizofanyika nchini Italia mwaka 1990.
Nusu fainali
Ufaransa ilishindwa katika nusu fainali mwaka 1958 na 1982, ilishinda kombe lake la kwanza na la pekee hadi sasa nyumbani mwaka 1998, na kisha kushindwa katika fainali mwaka 2006, dhidi ya Italia katika tukio lililokuja kuwa maarufu ambapo Zinedine Zidane alimpiga kichwa mchezaji wa Italia Mataranzzi.
Croatia ilishindwa na Ufaransa katika nusu fainali za mwaka 1998 katika fainali zake za kwanza kwa nchi hiyo tangu kuwa taifa huru baada ya kuvunjika kwa Yugoslavia.
Kikosi cha England kinamjumuisha mtu mwenye jina la utani . Jamie Vardy anamuita mchezaji wa timu ya taifa na timu ya Leicester City Harry Maguire kuwa ni kichwa pande , Slab head.
vardy alijiunga na waandishi habari na kuulizwa swali la mwisho. Jamie Vardy kutoka katika Vardy Express. Kichwa chako ni kikubwa kiasi gani?
Wakati Maguire alipofunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 siku ya Jumamosi dhidi ya Sweden, kelele zake za furaha zilikuwa kali sana na zilionekana kama anapiga keleza za kuumia.
Msjhambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku alipata jina la utani akiwa Manchester United, ambako wachezaji wenzake walifananisha kazi yake uwanjani na Sylvester