1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya Zanzibar Hereos kutocheza Soka

12 Desemba 2012

Chama cha Soka Zanzibar kimewasimamisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes.

https://p.dw.com/p/170NW
Picha: picture alliance/abaca

Visiwani Zanzibar, baada ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes kurudi na ushindi wa tatu kutoka michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati - CECAFA Tusker Challenge yaliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, Chama cha Soka cha Zanzibar ZFA, kimechukua uamuzi uliowashangaza wengi kwa kuwasimamisha wachezaji 14 wa timu hiyo kucheza soka kwa muda usiojulikana popote pale duniani kwa madai ya kuamua kugawana kiasi cha Dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya ushindi huo. Hivi punde Grace Kabogo amezungumza na Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji, ambaye kwanza alitaka amueleze iwapo uamuzi waliouchukua ni sahihi, ukizingatia kwamba wachezaji hao wameiletea nchi yao heshima.

(Kusikliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: Mohammed Khelef