1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Timu ya soka ya wanawake ya Uhispania yatajwa vinara duniani

15 Desemba 2023

Mabingwa wa Kombe la Dunia la Wanawake Uhispania wameorodheshwa wa kwanza duniani katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA, na kuwaondoa Sweden iliyokuwa inashikilia nafasi ya kwanza.

https://p.dw.com/p/4aDxy
Wachezaji wa kikosi cha timu ya soka ya wanawake ya Uhispania
Timu ya soka ya wanawake ya Uhispani ilinyakua ubingwa Kombe la Dunia la Wanawake mapema mwaka 2023.Picha: Zac Goodwin/empics/picture alliance

Mabingwa hao wa dunia wamekuwa timu ya nne iliyoshikilia nafasi ya kwanza baada ya Marekani, Ujerumani na Sweden.

Uhispania iliifunga Uingereza katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake mnamo mwezi Agosti, wakati huo ikipanda katika viwango vya ubora hadi nafasi ya pili.

Uhispania sasa inashikilia taji la timu bora duniani ya wanawake kufuatia matokeo mazuri waliyoyapata katika michuano ya hivi karibuni ya ligi ya mataifa ya Ulaya.

Timu ya wanawake ya Marekani imepanda hadi katika nafasi ya pili ikifuatiwa na Ufaransa kwenye nafasi ya tatu.

Ufaransa itachuana na Ujerumani katika nusu fainali ya michuano ya ligi ya mataifa ya Ulaya. Nao mabingwa wa Ulaya Uingereza, wametulia katika nafasi ya nne huku Sweden ikishuka hadi nafasi ya tano.