1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya soka Ujerumani kupewa zawadi nono

30 Novemba 2013

Wachezaji wa timu ya taifa ya kabumbu Ujerumani wameahidiwa marupurupu kama wataweza kufika katika robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil. Hiyo ni kuwapa motisha ya kulileta kombe la dunia nyumbani

https://p.dw.com/p/1AR4p
Picha: picture alliance/augenklick/GES

Shirikisho la soka la Ujerumani DFB limeahidi kutoa kiasi cha euro laki tatu (300,000) kwa kila mchezaji kama kikosi hicho kitashinda kombe la dunia.

Wachezaji pamoja na DFB walikubaliana jana Ijumaa kuhusu kile walichosema ni mfumo wa marupurupu ya mafanikio, sawa na yale waliyopata katika dimba la mwaka jana la Kombe la Mataifa ya Ulaya ambako walifika katika robo fainali.

Kila mchezaji atatia kibindoni euro 50,000 kama Ujerumani itafika robo fainali, laki moja katika nusu fainali na elfu mia moja hasmini kama watashindwa katika fainali. Mabingwa mara tatu wa Kombe la Dunia Ujerumani hawajalinyanyua kombe hillo tangu dimba la Euro 96. ukipewa ahadi kama hiyo huwa kunakuwa an msemo kuwa “heri punda afe lakini mzigo ufike”

Na wakati Ujerumani ikiahidi kuwapa marupurupu wachezaji wake, huko Barani Afrika, serikali ya Nigeria imeingilia kati pia kuyalipa madeni ya mshahara anaodai kocha wa timu ya taifa Stephen Keshi. Waziri wa michezo nchini Nigeria Bolaji Abdullahi amesema amepokea idhini kutoka kwa Rais Goodluck Jonathan kuyatatua masuala ya mishahara ya Keshi na wasaidizi wake, ambayo inafikia kiasi cha euro 357,000. Keshi, hajalipwa kwa karibu miezi mitano, hata baada ya kuisaidia timu ya taifa kunyakua kombe la Mataifa ya Afrika na kujikatia tikiti ya kucheza nchini Brazil.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Mohammed Dahman