1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya madaktari kuchunguza maradhi yasiyojulikana Marsabit

11 Mei 2023

Kufuatia ripoti za maafa ya watu tisa kutokana na ugonjwa usiojulikana.

https://p.dw.com/p/4RDaT
Kenia | Marsabit County | Impfung von Eseln
Picha: Michael Kwena/DW

Timu ya madaktari imetumwa katika eneo la Kargi jimboni Marsabit kaskazini mwa Kenya kufuatia ripoti za maafa ya watu tisa kutokana na ugonjwa usiojulikana.

Tisa hao walifariki katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wakati watu wengine themanini wakiendelea kupokea matibabu eneo hilo baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa wenyewe.

Wakaazi wa eneo hilo wanadai kuwa, mlipuko wa ugonjwa huo umeendelea kuwa kitisho kwao.

Mwakilishi wa wadi ya Kargi Christopher Ogom ameilaumu idara ya afya kwa kukosa kuwajibika licha ya ripoti kutolewa wiki mbili zilizopita.

Wakati huohuo, idara ya afya ya Marsabit imethibitisha kuwatuma maafisa wa afya katika eneo hilo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ugonjwa huo.

Awali, serikali ya kaunti ya Marsabit kupitia msemaji wake Barille Abduba ilikuwa imekana ripoti za mlipuko wa ugonjwa huo ikisema kuwa, yalikuwa ni magonjwa ya kawaida.