1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu kujitafutia tikiti za nusu fainali ya Champions League

7 Aprili 2014

Mabingwa Bayern Munich wanastahili kujipanga upya wakati watakapokutana na Manchester United siku ya Jumatano (09.04.2014) kujitafutia nafasi ya kucheza katika nusu fainali ya Champions League

https://p.dw.com/p/1BdQf
Champions League Manchester United - Bayern München
Picha: Reuters/Stefan Wermuth

Kocha wa Bayern Pep Guardiola anasema mchuano huo utakaochezwa uwanjani Allianz Arena, utakuwa kama finali, mchezo wa kufa kupona. Bayern waliutawala mkondo wa kwanza dhidi ya Manchester United lakini wakawekewa ulinzi mkali katika mchezo uliokamilika kwa sare ya goli moja kwa moja.

Guardiola aliwapumzisha mwishoni mwa wiki wachezaji wake nyota Franck Ribery, Arjen Robbem na nahodha Philipp Lahm. Lakini watakuwa bila ya huduma za Bastian Schweinsteiger na Javi Martinez ambao wanatumikia adhabu nao Thiago Alcantara na Xherdan Shaqiri wana majeraha.

Nao Borussia Dortmund watahitaji kuonyesha mchezo wa hali ya juu dhidi ya Real Madrid, kama ule waliocheza katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali walipowaduwaza Madrid magoli manne kwa moja nyumbani.

Baada ya kichapo cha magoli matatu kwa sifuri wiki iliyopita, Dortmudn wanamkaribisha Robert Lewandowski katika kile kinachoonekana kama mlima mkubwa wa kupanda. Cristiano Ronaldo atarejea katika kikosi cha kocha carlo Ancelotti baada ya kupona jeraha la goti.

CR7 anatarajiwa kurudi katika kikosi cha Carlo Ancelotti kitakachopambana nyumbani kwa BVB
CR7 anatarajiwa kurudi katika kikosi cha Carlo Ancelotti kitakachopambana nyumbani kwa BVBPicha: Getty Images

Mahasimu wa Real, Atletico Madrid wanawakaribisha Barcelona katika ngome ya Vicente Calderon, baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.

Atletico huenda watamkosa mshambuliaji Doego Costa aliyejeruhiwa katika mkondo wa kwanza. Atletico na Barca zimecheza mara nne msimu huu katika mechi ambazo zimekamilika kwa kutoka sare, huku magoli manne pekee yakifungwa.

Chelsea lazima wawazidi bguvu Paris St Germain, ambao watakuwa bila mchezaji Zlatan Ibrahimovich aliyejeruhiwa katiak mkondo wa kwanza ambao PSG iliibamiza Chelsea magoli matatu kwa moja. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ana matumaini kuwa mshambuliaji wake Samuel Eto'o atakuwa tayari kucheza baada ya kupona jeraha la misuli.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman