1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thulisile Nomkhosi Madonsela: "Mwanamke wa chuma"

Admin.WagnerD18 Mei 2016

Thulisile Nomkhosi Madonsela, mchunguzi wa ukiukwaji unaofanywa na serikali na taasisi zake nchini Afrika Kusini ametunukiwa Tuzo ya Wakfu wa Ujerumani kwa Afrika kutokana na mchango wake katika kutetea wanyonge.

https://p.dw.com/p/1Ipj4
BAlozi wa Ujerumani nchini Afrika Kusini Walter Lindner alimpa Madonsela habari za kuwa mshindi wa tuzo ya Ujerumani na Afrika kwa mwaka 2016.
Balozi wa Ujerumani nchini Afrika Kusini Walter Lindner alimpa Madonsela habari za kuwa mshindi wa tuzo ya Ujerumani na Afrika kwa mwaka 2016.Picha: Deutsche Afrika Stiftung e.V.

Kuna wale wanaomwita mama huyo kuwa ni mwanamke wa chuma wengine wanasema ni sauti kwa wale wasiokúwa nazo akiwa msimamizi wa utendaji wa serikali Madonsela amekuwa akifanya kazi bila ya kuchoka kuwalinda wananchi dhidi ya rushwa na taasisi za serikali na maafisa wasiokuwa na uwezo wa kufanya kazi.

Jambo hili limemfanya aheshimwe na watu walio mashuhuri nchini Afrika Kusini. "Juhudi za ofisi yake zimeitetea katiba kama sharia mama na kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliye au anapaswa kuwa juu ya sheria," anasema Profesa Njabulo Ndebele, mwenyekiti wa Mfuko wa Nelson Mandela, ulioanzishwa na marahemu Mandela mwenyewe.

Asimama kidete dhidi ya vigogo

Mama huyo wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 53 alichaguliwa katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka na Rais Jacob Zuma hapo mwaka 2009. Tokea wakati huo amekuwa akidai kuwepo kwa uwajibikaji sawa kutoka kwa wanyonge halikadhalika kwa vigogo vyenye ushawishi mkubwa kabisa.

Madonsela alimtaka raus Zuma kurejesha sehemu ya fedha alizotumiakukarabati makaazi yake binafsi.
Madonsela alimtaka rais Jacob Zuma kurejesha sehemu ya fedha alizotumia kukarabati makaazi yake binafsi.Picha: Getty Images/AFP/R. Jantilal

Miongoni mwa hatua zake za kishujaa kabisa ni kule kudai kwamba Rais Jacob Zuma alipe sehemu ya fedha za umma zilizotumika kukarabati makaazo yake binafsi. Hapo mwaka 2011 aligunduwa kwamba Idara ya Polisi ya Afrika Kusini iliingia kwenye mkataba kinyume na sheria jambo ambalo lilikuja kugharimu kazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi la Taifa Bheki Cele.

Hata kiongozi wa chama cha upinzani cha ukombozi wa kiuchumi Julius Malema hakuachiliwa hivi hivi na mwendesha mashtaka huyo wa serikali ambaye aligunduwa kwamba udhamini wa familia yake ulikuwa ukinufaika na isivyo stahiki kutokana na zabuni wanazopewa marafiki zake. Mwenyekiti wa Tume Uhuru ya Uchaguzi Pansy Tlakula naye ilibidi ajiuzulu hapo mwaka 2009 baada ya Madonsela kujuwa kwamba alikiuka taratibu za matumizi.

Wenyeji na wageni wamkubali

Wananchi wengi wa Afrika Kusini wanakubali kwamba amefanya kazi nzuri iliotia fora na hata wageni wamekuwa wakivutiwa nayae.Wolf Krug, mwakilishi wa kanda ya kusini mwa Afrika wa Wakfu wa Hanns Siedel ambalo ni shirika lisilo la kiserikalia Ujerumani lenye uwakilishi katika nchi takriban hamsini alitambua pia mchango wa Madonsela.

"Akiwa kama mwendesha mashataka wa serikali kwa nchi yake amejithibitisha mwenyewe kuwa ni mtu mahiri wa kulinda katiba ya nchi yake.Kutokana kutoyumba kwa msimamo wake kwenye wadhifa wake huo ameonyesha kwamba demokrasia ya Afrika Kusini iko hai kabisa," alisema Krug kumhusu mwanamama huyo.

Südafrika Thuli Madonsela Public Protector bei Presskonferenz
Thulisile Madonsela.Picha: Getty Images/AFP/G. Guercia

Madonsela mwenyewe ansema kujitolea kwake kupigania haki kumetokana na mfano wa Mzee Mandela ambaye anasema alikabiliwa na dhuluma kubwa. "Hata hivyo aliigeuza dhuluma hiyo kubwa dhidi yake kuwa mapambano ya kupigania haki ya kijamii kwa wote.Katiba yetu nzima imeasisiwa kutokana na mwamko wa wananchi walioteseka na dhuluma za kijamii na kuona inafaa wachukuwe hatua kukabiliana na hali hiyo."

Muda wa Madonsela katika ofisi yake unamalizika baadae mwaka huu. Lerato Mutaung ni mmojawapo wa vijana wa Afrika Kusini ambaye tayari analalamika juu ya kuondoka kwa mama huyo. "Mtu anayetakiwa kuchukuwa nafasi yako anatakiwa awe na sifa ya ofisi hiyo na kile kinachohitajika kwetu kuijenga nchi hii ya matumaini yetu."

Aitwa shushushu wa CIA

Hata hivyo kazi nzuri alioifanya Madonsela imepitia kwenye nyayo nyingi na sio kila mtu anaifurahia.Baadhi ya viongozi wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha (ANC) wamempachika jina kuwa ni shushu wa shirila la Ujasusi la Marekani CIA wakati vijana wa chama hicho wakimuita kuwa chale mjinga na mwanasiasa bandia.

Lakini sifa alizonazo mama huyo zinathibitisha kwamba wakosoaji wake hawako sahihi. Miongoni mwa sifa hizo ni kuteuliwa kwa binaadamu bora nchini Afrika Kusini kwa mwaka 2014 na mwanamke wa mwaka pamoja na mwanamke mwenye ujasiri mwaka huo huo. Msimmo wake wa kutokuwa na hofu umepelekea pia kutishiwa maisha yake mara kadhaa.

Mwandishi: Thuso Kumalo/Mohamed Dahman
Mhariri: Mohammed Khelef