Thailand yaanza maombolezo kifo cha Mfalme
14 Oktoba 2016Mfalme Adulyadej mwenye umri wa miaka 88 alifariki jana (14.10.2016) baada ya kuiongoza Thailand kwa miaka 70. Katika mji mkuu wa Thailand Bangkok wananchi wamejipanga kandoni mwa barabara katika eneo linalotazamiwa kupita msafara unaobeba jeneza la mfalme Bhumibol Adulyadej kutoka hospitali ya Siriraj hadi hekalu la Wat Phra.
Mnamo mwongo mmoja uliopita hali ya afya ya mfalme Adulyadej haikuwa nzuri na mara nyingi alikuwa amelazwa hospitalini kutokana na magonjwa tofauti.Wengi walitazamia kifo chake japo kwa wasiwasi mkubwa. Katika kipindi cha maombolezi serikali imewaomba wananchi kuvalia nguo za heshima na zinazodhihirisha majonzi. Wengi walioko barabara za mji wa Bangkok ambao ndio mji mkuu wa Thailand wamevalia mavazi ya rangi nyeusi. Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kuwa mfalme mpya kwa mujibu wa katiba, lakini ameomba shughuli ya kurithi madaraka icheleweshwe kidogo.Mwanamfalme hyo mwenye umri wa miaka 64 hajafahamika sana na raia wa Thailand na hajapendwa sana na raia kama babake. Ameishi muda mwingi nje ya nchi na hasa Ujerumani
Bendera zote kupeperushwa nusu mlingoti
Serikali imetaka shughuli za burundani kusitishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja tu ili kuzuia kuvurugika uchumi wa taifa. Utalii ni mojawapo ya sekta zinazoiletea kipato cha Thailand na burundani ni kiunga muhimu. Baraza la mawaziri limetanga leo kuwa siku ya mapumziko na bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti katika siku 30 zijazo.
Nao viongozi mbalimbali duniani wamekuwa wakituma risala zao za rambirambi akiwemo rais wa Marekani Barack Obama,ambae alisema mfalme Adulyadej atakumbukwa kama mtu aliyewajali watu wake na kuboresha hali kwa vizazi vijavyo.Nae rais Francois Hollande alimmininia sifa tele mfalme Adulyadej akimtaja kuwa mtu mwenye utu na aliyezingatia haki .
Ingawa nafasi ya mfalme inatambuliwa tu na katiba amekuwa kiungo muhimu katika kiuwapatanisha wanasiasa kunapotokea vurugu. Lakini katika siku za hivi karibu alilemewa na majukumu yake baada ya kukabiliwa na tatizo la figo,akili, mapafu, moyo na hata damu. Hata alijtenga na vurugu za kisiasa za hivi karibuni yakiwemo mapinduzi aliyomweka generali mkuu wa jeshi madarakani.Mara ya mwisho kuonekana hadharani alikuwa katika kiti cha magurudumu.Aliwapungia mkono wannachi japo alionkana dhaifu.
Mwandishi:Jane Nyingi/APE/AFPE
Mhariri: Gakuba Daniel