TEXAS:Bush ataka NATO igawane mzigo wa kupambana na Taliban
22 Mei 2007Rais George Bush wa Marekani amewataka wanachama wa Umoja wa NATO kubeba kwa pamoja jukumu la kupambana na wapiganaji wa Kitaleban huko Afghanistan.
Akizungumza na Katibu Mkuu wa NATO,Jaap de Hoop Scheffer, katika shamba lake huko Texas, Rais Bush amesema kuwa ni lazima majeshi ya NATO yabadilike kuweza kupambana na vitisho vya hivi karibuni vya wapiganaji wa Taliban.
NATO inawanajeshi kiasi cha elfu 35 wanaopambana na waasi wa kitaliban huko Afghanistan.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa NATO alilaumu mbinu za Wataliban, kuwatua raia kama ngao, ya kwamba zimesababisha kuongezeka kwa vifo vya raia hivi karibuni.
Mashambulizi ya anga ya majeshi hayo yamekuwa yakisababisha vifo vya raia.
Wakati huo huo, maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa majeshi ya nchi hiyo na yale ya NATO yamefanikiwa kuwaaua watu 25 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Taliban, baada ya mapambano ya 14 huko kusini mwa nchi hiyo.