1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi lasababisha uharibifu mkubwa New Zealand

4 Septemba 2010

Maafisa wametangaza hali ya hatari kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika mji wa Christchurch nchini New Zealand mapema leo asubuhi.

https://p.dw.com/p/P46S

Mji huo ulio mkubwa wa pili nchini New Zealand,umeharibiwa vibaya sana. Kuambatana na maafisa wa mji huo, hakuna vifo vilivyoripotiwa lakini watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya. Katikati ya mji wa Christchurch ulio na wakaazi wapatao laki tatu na nusu, kuta za majengo ya zamani ziliporomoka, huku zikiangukia magari na kuziba barabara kadhaa.

Tetemeko hilo lililotokea mapema leo alfajiri, kilomita 30 Magharibi mwa mji wa Christchurch, lilisababisha kupotea kwa umeme katika maeneo kadhaa pamoja na kuharibu mabomba ya maji taka. Uwanja wa ndege wa Christchurch ulio katika kisiwa cha kusini, ulifungwa hapo awali lakini sasa umeshafunguliwa kwa misafara. Wakati huo huo, mtandao wa reli na madaraja katika kanda hiyo yanakaguliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo la ardhi.

Mwandishi: Issa,Munira Mohamed Yusuf/ZPR