Tel Aviv. Kiongozi mpya wa chama cha Labour ataka uchaguzi na mapema.
11 Novemba 2005Matangazo
Nchini Israel , kiongozi mpya wa chama cha Labour Amir Peretz amesema kuwa anampango wa kumtaka waziri mkuu Ariel Sharon kupanga tarehe ya uchaguzi na mapema.
Radio ya Israel imeripoti kuwa Peretz na Sharon wanatarajiwa kukutana kulijadili suala hilo hapo siku ya Jumapili.
Hii inakuja siku moja baada ya Peretz kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Labour, akimwangusha makamu waziri mkuu Shimon Peres.
Peretz amesema kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa akiwa kiongozi wa chama cha Labour , anampango wa kukiondoa chama chake kutoka katika serikali ya mseto inayoongozwa na Sharon na chama chake cha Likud, ili kulazimisha uchaguzi na mapema.