Uchumi
Teknolojia kurahisisha manunuzi ya serikali
3 Novemba 2017Matangazo
Wajumbe kutoka mamlaka za manunuzi ya umma Afrika Mashariki wamekamilisha kongamano lao la kumi mjini Kampala, Uganda, adhuhuri ya leo ambapo wamejadili mada ya kuhusisha teknolojia katika michakato ya matumizi ya fedha za serikali zao pamoja na jumuiya hiyo. Miongoni mwa hoja zilizoibuka katika mashauriano yao ya siku tatu ilikuwa jinsi teknolojia itakavyorahisha shuguli zao kwa uwazi na wakati huku mienendo ya ufisadi ikipunguzwa. Mwandishi wetu Lubega Emmanuel amezungumza na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania, Balozi Matern Lumbanga, ambaye ameanza kwa kufafanua umuhimu wa kongamano hilo la kila mwaka.