1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran yashikilia kuendelea na mpango wake wa nyuklia

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPd

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad anashikilia kuwa nchi yake haitampa nafasi mtu yoyote kuingilia haki yake ya kuwa na mpango wa nuklia.Tamko hilo linatolewa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia shughuli za kutumia nishati ya Nuklia IAEA linajiandaa kutoa ripoti kuhusu mpango wa nuklia wa Iran unaozua utata.

Rais Ahmedinejad anatoa kauli hiyo baada ya muda wa mwisho uliowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wa kusitisha mpango huo wa kurutubisha madini ya uranium kuisha.Mpango huo wa kurutubisha madini ya uranium unazalisha nishati japo unaweza kuimarishwa na kutengeza silaha za nuklia.

Marekani kwa upande wake inadai kuwa mpango huo unalenga kutengeza bomu la atomiki jambo ambalo Iran inakataa katakata na kusisitiza kuwa wanaazma ya kutengeza nishati ya nuklia pekee.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huenda likaamua kuibana Iran zaidi na kuiwekea vikwazo vikali kufuatia uamuzi wake wa mwaka jana wa kuiwekea vikwazo vichache hususan katika shughuli za nuklia.