TEHRAN.Iran kuendeléa kurutubisha madini ya Uranium
26 Machi 2007Matangazo
Iran imesisitiza kuwa haitasimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium licha ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo vipya na baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Msemaji wa serikali ya Iran amesema pia nchi yake itaweka mipaka katika uhusiano wake na tume ya umoja wa mataifa inayosimamia nishati ya atomiki.
Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa hivi majuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kuweka vikwazo vya silaha na kiuchumi kwa baadhi ya watu binafsi na taasisi mbali mbali za Iran.
Wakati huo huo Iran inapanga kuwafungulia mashtaka ya kuvuka mpaka katika pwani ya nchi hiyo bila ruhusa wanamaji 15 wa Uingereza waliokamatwa mwishoni mwa wiki.