TEHRAN:Bunge laidhinisha uteuzi wa mawaziri wa Mafuta na Viwanda
14 Novemba 2007Matangazo
Bunge nchini Iran linaidhinisha uteuzi wa mawaziri wa Mafuta na Viwanda uliofanywa na Rais Mahmoud Ahmedinejad hatua inayodhaniwa kumuongezea madaraka katika usimamizi wa uchumi nchini humo.Bunge hilo linaidhinisha uteuzi wa Gholam Hossein Nozari waziri mpya wa Mafuta vilevile Ali Akbar Mehrabian waziri mpya wa Viwanda.Viongozi hao walikuwa wanakaimu nafasi hizo tangu mwezi Agosti.