TEHRAN: Maafikiano yapatikana kati ya Iran na IAEA
13 Julai 2007Matangazo
Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA limesema kuwa limekubaliana na Iran njia ya kusuluhisha masuala mengine yanayohusika na majeribio yake ya zamani ya plutonium.Baada ya majadiliano ya siku mbili mjini Tehran,shirika hilo limepanga ziara ya wakaguzi wake nchini Iran.Tume ya wakaguzi wa IAEA,itatembelea mtambo wa utafiti wa kinyuklia wa Arak,mwishoni mwa mwezi wa Julai.Maamuzi kuhusu njia za kulinda mtambo wa kurutubisha uranium huko Natanz yatajadiliwa mapema mwezi wa Agosti.Madola ya Magharibi yanatuhumu kuwa mradi wa nyuklia wa Iran una azma ya kutengeneza silaha za nyuklia. Lakini serikali mjini Tehran inakanusha madai hayo na inasema,inataka teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya kuzalisha nishati tu.