TEHRAN: Iran yatishia kulisusia shirika la IAEA
14 Juni 2007Matangazo
Iran imetishia itawacha kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia nishati ya kinyuklia, IAEA, iwapo itawekewa vikwazo vipya.
Balozi wa Iran wa shirika la IAEA ametoa tangazo hilo baada ya mkutano wa halmashauri ya shirika hilo uliozungumzia mradi wa Iran wa nishati ya kinyuklia.
Balozi huyo amesema nchi yake imepata uzoefu mkubwa wa kurutubisha madini ya Uranium na mataifa makuu ya ulimwengu yanapaswa kuikubali hali halisi ya mambo.