TEHRAN: Iran yakataa katakata kusimamisha mradi wake wa nyuklia
31 Mei 2007Matangazo
Iran imesema katu haitaridhia matakwa ya mataifa ya magharibi kuhusu mradi wake wa nishati ya nyuklia.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Mohammad Ali Hosseini amesema Iran haitakubali kusimamisha mradi wake huo ambao mataifa ya magharibi yanachelea huenda serikali hiyo ikautumia kutengeneza silaha za kinyuklia.
Msemaji huyo amesema Iran itafuata taratibu zote za kisheria kutetea haki yake ya kuuendeleza mradi huo.
Wakati huo huo, mpatanishi mkuu wa mradi wa kinyuklia wa Iran, Ali Larijani, anatarajiwa kukutana na mkuu wa sera za kimataifa wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, kujaribu kutanzua mzozo kuhusu mradi huo wa Iran:
Serikali ya Iran imekuwa ikisisitiza mradi wake ni wa matumizi salama.