1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran itaanza kurutubisha madini ya uranium juma hili

8 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmv

Iran imesema itaanza tena kurutubisha madini ya uranium juma hili na kwamba haina wasiwasi wowote juu ya uwezekano wa kuwekewa vikwazo iwapo itafikishwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa. Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zimeitisha mkutano wa dharura wa magavana wa bodi ya shirika la kimataifa la nishati ya atomiki hapo kesho kujadili kesi ya Iran.

Mataifa hayo ambayo yamekuwa yakiongoza mazungumzo kati ya serikali ya Tehran na umoja wa Ulaya, yatapendekeza Iran ifikishwe mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa, ikiwa itaendelea mbele na mpango wake wa kuanza tena shughuli za nuklia katika kinu cha Isfahan.

Iran imesema itaanza shughuli zake katika kiwanda cha Isfahan mara tu vifaa vya ukaguzi vya shirika la kimataifa la nishati ya nuklia, vitakapokamilika.