1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Putin na Ahmedinejad kujadili mradi wa nyuklia wa Iran

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FG

Rais Vladimir Putin wa Urusi amekwenda Teheran kujadiliana na Rais Mahmoud Ahmedinejad,mradi wa kinyuklia wa Iran uliozusha mabishano.Siku ya Jumatatu,Putin alipinga kuiwekea Iran vikwazo vikali zaidi.Kwa upande mwingine,waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates,kwa mara nyingine tena ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuwa na msimamo mmoja kuhusu mgogoro wa nyuklia wa Iran.