TEHERAN : Iran yatarajiwa kutoa jibu juu ya mpango wake wa nyuklia!
29 Agosti 2006Matangazo
Jumuiya ya Kimataifa leo inasubiri jibu la Iran juu ya pendekezo la jumuiya hiyo la kuitaka Iran iache kurutubisha madini ya uranium.
Rais wa nchi hiyo bwana Mahmoud Ahmadnejad anatazamiwa kutoa jibu hilo wakati zimebaki saa chache kabla ya muda uliotolewa na Umoja wa Mataifa kumalizika.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeipa Iran muda wa hadi tarehe 30 ya mwezi huu yaani kesho, ili iache mpango wa kurutubisha madini ya uranium.
Baraza hilo limesema litaiwekea Iran vikwazo ikiwa haitaacha mpango huo hadi hapo kesho.