TEHERAN: Iran yadai kuwakamata raia wake waliokuwa wakiendesha ujasusi kwa ajili ya CIA
6 Januari 2004Matangazo
Gazeti mashuhuri la Iran linalochapishwa kila siku, Jomhouri Eslami, katika toleo lake la leo linasema majasusi wengi raia wa Iran ambao walikuwa wakilipelekea shirika la ujasusi la Marekani CIA taarifa, wamekamatwa na idara za usalama za Iran. Gazeti hilo limemunukulu mwenyekiti wa baraza kuu la kisheria jeshini, Mohamed Niazi, akisema adui anataka kujipenyeza miongoni mwa jeshi letu ili kulidhofisha na kuwahonga makamanda wetu.
Gazeti hilo Jomhouri Eslami, ambalo linaelezewa kuwa na mafungamano na wahafidhina wenye sera kali za kidini, linasema Bwana Mohamed Niazi ameyasema hayo wakati wa mkutano na viongozi wa kidini katika jeshi la Iran, katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Iran wa Machhad.
Matamshi hayo ya kiongozi wa baraza kuu la sheria katika jeshi la Iran yanatokea mnamo wakati kulikuwepo tetesi kwamba huenda uhusiano wa Iran na Marekani utakua mzuri, baada ya Marekani kupeleka waokozi katika eneo la Bam la kusini mwa Iran, lilikumbwa tetemeko la ardhi. Matamshi pia yanatokea mnamo wakati ambako wakuu wa Iran wanasema wanajiandaa kukituma chombo cha kwanza cha nchi hiyo cha Satalite angani, mnamo muda usiozidi miezi kumi na minane ijayo.