TEHERAN: Iran yadai kuendelea kurotubisha madini ya uranium
28 Oktoba 2006Matangazo
Shirika la habari la nchini Iran, ISNA, limesema Iran imeendelea na kazi yake ya kurotubisha madini ya uranium katika kinu cha pili na hivyo kupanua mpango wake ambao nchi za magharibi zinaituhumu kutaka kutengeneza bomu za kinyuklia. Rais wa Marekani George W. Bush, amesema ni budi jumuiya ya kimataifa iongeze juhudi mara dufu ili kuisimamisha Iran isipate nguvu za kinyuklia. Hata hivyo, waziri wa ulinzi wa Rushia Sergei Ivanov, amesema ni mapema mno kuzungumzia Iran kuweza kutengeneza silaha za kinyuklia na kwamba sio jambo la kutia wasi wasi.