Michoro ya Grafiti ni kitu kipya jiji la Dar es Salaam. Katika miaka ya 1970 vijana wengi walikua wakitumia vipande vya mkaa na kuchora majina yao kwenye kuta kote katika jiji hili. Alama zao zilikuwa zikiitwa chata na hivi sasa kama ilivyokuwa huko nyuma vijana bado wanaacha alama kwa kuandika majina yao kwenye kuta katika miji yao kama njia ya kuacha kumbukumbu.