Shinikizo la damu ni tatizo la kawaida la kiafya ambalo lisipodhibitiwa au lisipotibiwa huweza kuathiri ubongo, moyo, figo na hata kusababisha kiharusi miongoni mwa matatizo mengine ya afya. Visa vingi vya shinikizo la damu hutokea Afrika au miongoni mwa watu wenye mizizi ya Afrika. Kwenye vidio hii ya Kurunzi Afya, tunaangazia tatizo hilo na namna ya kudhibiti au kuishi na shinikizo la damu.