1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tatizo la ajira ya watoto huenda likamalizika katika kipindi cha muongo mmoja

Saumu Mwasimba4 Mei 2006

Shirika la kimataifa la ajira duniani ILO limesema kwamba idadi ya ajira ya watoto imepungua kwa kiwango kikubwa

https://p.dw.com/p/CHnO

Kwa mujibu wa shirika hilo, ikilinganishwa na idadi ya ajira ya watoto ya miaka minne iliyopita tatizo la ajira ya watoto limepungua kwa asilimia 11 hadi kufikia milioni 218 kwa watoto kati ya miaka 5 hadi 17.

Shirika hilo pia linasema idadi ya watoto wanaoajiriwa katika kazi ngumu ambapo hali yao ya kimwili na kiakili inakuwa hatarini imepungua hadi asilimia 26 na kufikia milioni 126.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la kimataifa la ajira duniani,Juan Somavia amesema kumalizika kwa tatizo la ajira ya watoto kuko mikononi mwetu.licha ya kwamba vita dhidi ya ajira ya watoto limebakia kuwa tatizo kubwa lakini tuko kwenye mkondo barabara.

Kazi hatari zaidi ni za ukulima,uchimbaji migodi na ujenzi lakini pia miongoni mwa kazi hizo ni utumwa,ukahaba na kuingizwa jeshini watoto.

Ripoti ya shirika la ajira duniani ILO inaeleza pia tatizo la ajira ya watoto imepungua kutokana na kuongezeka kwa nia ya kisiasa ya kukabiliana na hali hii na hasa katika mataifa makubwa yanayoendelea kama vile Brazil na China pamoja pia na uchumi imara duniani ambao unapunguza haja ya familia maskini kuwatuma watoto wao kufanya kazi.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la ILO barani Afrika kusini mwa jangwa la sahara bado tatizo la ajira ya watoto lip o ambako asilimia 26 au watoto millioni 50 wanafanya kazi.

Kiasi cha mataifa 160 asilimia 90 ya nchi wanachama wa shirika hilo la ajira duniani ILO,yamepitisha mkataba wa mwaka 1999 juu ya ajira ya watoto,kutoka idadi ya 117 miaka mine iliyopita.

Idadi ya nchi zinazozingatia mkataba wa mwaka 1973 wa kuweka umri wa miaka 15 kuwa kama kiwango cha chini cha kuajiriwa kazi imeongezeka na kufikia hadi zaidi ya 140 kutoka 116.

Amerika ya kusini na Carribean yamepunguza kwa kasi tatizo hili katika kipindi cha miaka mine iliyopita ambapo idadi ya watoto walioajiriwa imepungua kwa zaidi ya asilimia 60.Hivi sasa ni asilimia 5 pekee ya watoto wanaofanyishwa kazi.

Nchini Brazil ambako rais Luiz Inacio Lula Da Silva mwenyewe alikuwa akifanya kazi akiwa motto,idadi ya watoto wanaofanya kazi wakiwa na umri kati ya 5-9 imepungua hadi asilimia 61 tangu mwaka 1992 wakati ajira ya watoto wenye umri wa miaka kati ya 10-17 imepungua hadi asilimia 36.

Maeneo ya Asia na Pacific pia idadi hiyo imepungua lakini bado kuna watoto milioni 122 wanaofanya kazi nah ii imefanya eneo hilo kuwa lenye idadi kubwa kabisa ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 14 wanaofanya kazi.