Katika makala ya 'Maoni mbele ya Meza ya Duara', safari hii kipindi hiki kinapiga darubini miaka mitano nyuma wakati mamia kwa maelfu ya wakimbizi walimiminika Ujerumani naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema ‘Tunaweza‘ akimaanisha wanaweza kuwahudumia wakimbizi. Je sera hiyo imefanikiwa kwa kiwango gani? Josephat Charo ndiye nahodha wa kipindi kwa leo.