Mila za kukeketa watoto wa kike nchini Tanzania bado zinashika kasi licha ya elimu ya kupinga mila hizo kuendelea kutolewa hasa na mashirika binafsi. Miongoni mwa mikoa inayotajwa kuongoza kwa vitendo hivyo ni mkoa wa Mara. Mwaka 2016 zaidi ya mabinti 800 wa Wilaya ya Tarime pekee walikeketwa huku wengine 300 wakikimbia majumbani mwao kwa kuogopa kukeketwa.